MTAMBUE Sirkiller MC KWA UFUPI



Jina; Sirkiller MC
KaziEMCEE / SONGWRITER / ACTOR / TANZANIAN RAP`S UPPER ECHELON

Miaka;24

Anapoishi; Kiwalani M/Mirefu

Namba; 0719-115037

FacebookSirkiller Mc

Twitter: SirkillerMC

Instagramsirkillermc

Email: sirkillermichano@gmail.com

>>PAKUA MIZIKI YAKE HAPA<<





0 Comments:

HII HIWE FUNDISHO KWA WENGINE

 Angalia Picha Hizi Kwa Makini











0 Comments:

DOWNLOAD NEW TRACK TOKA KWA PURE MC- KULA KONA

  • Msanii  toka kundi la VVM yani Vina Vinaongea Music PURE MC ameachia track yake mpya Hiitwayo ''KURA KONA'' Ili kuisikiliza>>>DOWNLOAD HERE



0 Comments:

NUNUA WIMBO WA ''Maarifa Bigthinker'' HAPA


Sapoti harakati kwa kununua wimbo wa Maarifa Bigthinker .feat.Syllabus Sahihi & Maarifa NAC - YALIYOMO ..chini ya Prod_Lezzy
 




0 Comments:

HAPPY BIRTHDAY MC LOVE

Msanii wa miziki ya VIGODOLO toka kundi jipya la MAVOCO LIST leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa
Jina Halisi: BONIFASI LIPONDA
Jina la Sanaa; MC Love
Kazi: Music/Bahdela Company Limited
Tarehe Ya Kuzaliwa; 14/2/1986
mahali Anapoishi;Kiwalani Minazi Mirefu
mpaka sasa ni baba wa watoto wawili ''JANE na TINA''


ENZI HIZO



SASA 

Ilikujua mengi kuusu MC LOVE gusa link hii>>> MC Love TZ

0 Comments:

DOWNLOAD NEW TRACK TOKA KWA ''MIKA MBWAI'' Awaamini

Wimbo huu umefanyika PLEXITY REC ulipofanyika wimbo wa Kala Jeremiah SIKATI TAMAA chini ya Prod ZEST ..Sikiliza Wimbo Wa MIKA MBWAI  Hapa aliomshirikisha SOPRANO na kaka yake MON G mtoto Wa Dar>> DOWNLOAD HERE

0 Comments:

ALICHOKIPOST ''NIKKI MBISHI'' KWENYE UKURASA WAKE WA INSTAGRAM HIVI KARIBUNI

"Nimefiwa na baba mdogo (last born wa marehemu baba yangu),mama mdogo,kaka,uncle na watoto wa kaka yangu.Wameungua na moto usiku wa kuamkia leo".Aliripoti @stereotanzania
#POLE_STEREO

0 Comments:

UTANGULIZI KATIKA KITABU CHA "JIFUNZE KUCHANA"


Rap (uchanaji) ni nguzo ambayo imo katika utamaduni wa Hip Hop. Nguzo za Hip Hop kwa mujibu wa Africa Bambataa (cited in Hanzi, 2012) zinatajwa kuwa nguzo za Hip Hop ziko Tano (Machata, Udijei, Uchanaji, Mabreka na Maarifa) lakini kwa mujibu wa UN (2001) kupitia azimio la amani la Hip Hop lililopitishwa na wanaharakati zaidi ya 300 wa Hip Hop na mashirika na taasisi nyinginezo zinaongezea nguzo nne (Ujasiriamali, Mitindo ya Mtaani, Lugha ya mtaani na midundo kinywa). Hali hii inafanya kuwepo kwa makundi mawili yanayoamini kuwa nguzo za Hip Hop ni tano na yanayoamini nguzo za Hip Hop zimeongezeka na kuwa Tisa.
Rap kwa Kiswahili sanifu huelezewa kama ni kitendo cha ku – “sema kwa ghafla au kwa ukali” (Tuki, 2000). Kuna uwezekano mkubwa hii imetokana na uwiano, kwamba maelezo haya yatakuwa yametokana na ile tafsiri ambayo Bahati (2011) anayosema kuwa “Muziki huu ulikuwa unaitwa “muziki wa kufokafoka” kipindi hicho”. KBC (2008) anasema “Neno kufoka foka ni neno la kibaguzi kwa wachanaji kama neno ‘N’ kwa mtu mweusi.. Neno hilo lilianzishwa na waandishi wa habari wa kitanzania wenye uelewa mdogo na wasiojua chochote kuhusu muziki wa Rap na hata walipoelezewa vizuri waligoma kuuita unavyopaswa (Muziki wa Rap) wakaamua kuuita Muziki wa kufoka foka.
Tafsiri sahihi ya Rap inaelezewa na Bahati (2011) anaposema “hilo jina (kufoka foka) halikuwa sahihi, na uliupa mziki huu taswira mbaya. Lakini kwa kuwa ulikuwa ni muziki mpya, inawezekana hatukujua jina gani litakuwa sahihi… Muziki huu ulionekana ukiwa na hiyo dhana ya kufokafoka, na kawaida ya tamaduni zetu, mtoto hamfokei mzazi. Hivyo inawezekana Hip Hop ikaonekana ni muziki unaochochea uasi dhihi ya tamaduni zetu…. neno sahihi la Kiswahili ni kughani” au Michano (kuchana) kwa mujibu wa zavara (2012).
Kwa tafsiri hizo, ni wazi kwamba mtu anayefanya muziki wa Rap au “Rapper” kwa Kiswahili huitwa Mchanaji au Mghanaji. Hivyo katika kitabu hiki nitatumia neno Mchanaji kumaanisha Mghanaji au “Rapper”. Rap na Hip Hop inaonekana kama ni maneno mbadala kwamba neno Rap humaanisha Hip Hop na neno Hip Hop humaanisha Rap. Ukweli ni kwamba “Rap na Hip Hop sio maneno mbadala” (Dubois na Bradley, 2010). Kiuhalisia, Rap ni Moja kati ya nguzo zinazounda Utamaduni wa Hip Hop hivyo Rap ni kijisehemu cha Hip Hop, Zavara (2012) anasema “kipengele cha michano ndicho kinachovuma sana….. na kufanya hata Baadhi ya watu kufikiri kuchana ndio Hip Hop.
Ni ukweli usiopingika kwamba sio kila mwenye uwezo wa kuchana anaweza kuwa ni Mchanaji wa Hip Hop japo Muziki wa Rap hujengwa kwa uchanaji. Kwa kawaida mchanaji wa Hip Hop huitwa “Mc” na mchanaji wa kawaida huitwa “Rapper” na hii ndiyo sababu hata katika aina nyingine za muziki kwa Mfano: dansi kuna marapa.
Stic Man (cited by Zavara, 2012) anasema, “Ni kama vile kuwe na mpiganaji wa mapigano ya kitaa na mtu aliyefunzwa na kufuzu sanaa ya mapigano”. Kawaida mpiganaji wa mtaani ni mpiganaji, lakini huyu aliyefuzu na mfanyaji mazoezi ya sanaa ya mapigano anakuwa na uwezo wa ziada. Huu mfano ndio tofauti kubwa iliyopo kati ya mchanaji wa kawaida na MC (Zavara, 2012).
Mchanaji wa kawaida (Rapper) ni yule mchanaji mwenye uwezo wa kuchana ambaye hana uelewa kuhusu utamaduni au mwenye uelewa kuhusu utamaduni wa Hip Hop lakini hafuati au hachani katika Misingi, kanuni na taratibu za uchanaji katika utamaduni wa Hip Hop lakini Mchanaji wa Hip Hop (Mc) ni yule mchanaji mwenye uwezo wa kuchana kwa kufuata misingi, kanuni na taratibu za uchanaji zilizopo katika utamaduni wa Hip Hop.
Myka 9 (quoted in Edwards, 2009) wa Freestyle Fellowship anasema anasema kuwa “wachanaji wa sasa wamejengwa kutokana na misingi ambayo iliyoachwa ”. Hapa tunaona kwamba kuna neno “Misingi” ambayo inaweza kuwa Misingi ya Uandishi na Misingi ya Hip Hop. Neno “Iliyoachwa” ni wazi limeficha nomino Fulani, ukisikia neno “Iliyoachwa” ni lazima ujiulize maswali mawili. (a) ni ipi iliyoachwa na (b) ni kina waliyoiacha. Swali la kwanza jibu lake itakuwa iliyoachwa ni misingi na waliacha misingi hiyo ni waliotangulia kwa maana ya wakongwe. Hivyo ili ujifunze Misingi ni lazima ujifunze kutoka kwa waliotangulia kama P The Mc (personal communication, 2014) anavyosema “Ukiwa na ndoto ya kuwa Mc ni vema ukawaona watu waliokutangulia, ukawaomba ushauri juu ya kitu gani ufanye ili uweze kuwa mchanaji mzuri”.
Kitabu Hiki kimelenga kuelezea vitu ambavyo ni muhimu mchanaji awe navyo ili aweze kuwa Mchanaji wa Hip Hop kama ambavyo tumekwishaona kwamba kuweza tu kuchana hakumfanyi Mchanaji kuwa mchanaji wa Hip Hop. Kitabu hiki kinahusisha taarifa kutoka katika vitabu, makala, maazimio, dokumentali, wanaharakati, nyimbo za wasanii, mahojiano na mbinu nyinginezo ukusanyaji wa taarifa. Imani yangu ni kwamba msomaji ataweza kujifunza mambo mengi yahusuyo sanaa ya uchanaji katika utamaduni wa Hip Hop.
kimeandikwa na
Malle Marxist
© 2014
KINAPATIKANA
Mawasiliano: 0715076444

0 Comments:

HIP HOP INA NGUZO WABONGO HAMZIWEZI

Wakati Madee alipotoa kibao cha “Hip Hop Haiuzi”. Kila mwanahiphop alikuwa na neno lake aliloweza kulizungumza. Wachanaji wengi wameshamchana katika nyimbo zao tangu kibao kimetoka mpaka leo anaendelea kuchanwa hata wachanaji wanaochipukia. Katika kibao hicho kuna mahali Madee anasema “Hip Hop ina Nguzo, bongo hamziwezi”. Ni kauli nyepesi kuitamka lakini ukitumia mawanda mapana ni ngumu kuifafanua ikaeleweka katika maana mahsusi kutokana uelewa wa Moja moja uliopo .
Katika kujadili kauli hii “Hip Hop ina nguzo, bongo hamziwezi” nitatumia maswali mawili kufafanua kauli hii. Swali la kwanza ni “Je Hip Hop ina nguzo, Nguzo za Hip Hop ni zipi” na la pili “Je ni kweli nguzo hizo za Hip Hop wabongo hawaziwezi?”. Nitatumia maswali hayo kupima usahihi na uhalali wa kauli hiyo.
Swali la kwanza. “Madee alisema kwamba “Hip Hop ina Nguzo”. Ni kweli kabisa alikuwa sahihi kusema hivyo. Katika kitabu changu cha “Chuo Kikuu cha Hip Hop” niliandika kwamba mwanzoni nguzo za Hip Hop zilitajwa na Africa bambataa kuwa ni nne ambazo ni Machata, Mabreka, Uchanaji na Udijei. Nguzo nyingine iitwayo Maarifa iliongezeka na kuzifanya ziwe tano.
Katika azimio la amani la Hip Hop (Hip Hop Declaration of Peace) lililofanyika katika umoja wa mataifa (UN) mwaka 2001 na kusainiwa na wanaharakati na taasisi mbalimbali zaidi ya 300 waliongeza nguzo nne ambazo ni “Ujasiriamali wa mtaani, Mitindo ya mtaani, Midundo kinywa na Lugha ya mtaani” na kuzifanya nguzo za Hip Hop kuwa Tisa.
Hata hivyo bado kuna mgongano wa hoja kutokana na kuwepo kwa pande mbili ambzo zinaamini nguzo za hip hop ni tano na upande mwingine ukiamini nguzo za Hip hop zimeongezeka na kuwa Tisa.
Swali la pili ambalo linauliza “Je ni kweli nguzo hizo za Hip Hop wabongo hawaziwezi?” ni swali ambalo linanifanya nijiulize maswali mengine mengi. Kama ambavyo nimekwisha kuelezea na kuzitaja Nguzo za Hip Hop hapo juu.
Nachojaribu kuelewa, hii ni namna nyingine kusema kwamba “wabongo hatuwezi kuwa wachanaji, wabongo hatuwezi kuwa madijei, wabongo hatuwezi kuwa mabreka, wabongo hatuwezi kuwa wachata, wabongo hatuwezi kuwa na maarifa, wabongo hatuwezi kuwa wajasiriamali, wabongo hatuwezi kupiga Midundo kinywa na wabongo hatuwezi kufanya mitindo ya mtaani.
Nikimuuliza mtu kama Mejah Mbuya kwamba wabongo hatuwezi kuwa wapiga machata nafikiri atanijibu… “Nenda Ubalozi wa Uingereza.. ukawaulize wale wazungu kwanini walikubali ukuta wao tuupige machata..”. ama nikamuulize Dj Bony Luv kwamba “wabongo hatuwezi kuwa madijei” lazima ataniuliza “..kwani wewe umenifahamu vipi..?”
Inawezekana Madee akawa anamkubali Mc mmoja tu Tanzania mpaka sasa kwa maana kuna nyakati (kama sio mwaka jana basi mwaka huu) alishawahi kusema anamkubali sana Nash Mc na ndiye mc wa kweli anayefanya hip hop Tanzania..
Napata shida kupata usahihi wa kauli hii… kwamba “Hip Hop ina Nguzo wabongo hawaziwezi” huenda mchanaji alikuwa na maana yake mahsusi ambayo ni tofauti na hii ambayo nimeielezea hapo juu.. usiangalie Chini…. NIMEANGUSHA CHENCHI….
Imeandikwa na
Malle Marxist
0715076444
©2014

0 Comments:

NJIA RAHISI YA KUPATA MIXTAPE YA P The MC na ZaiiD ''MWENGE+KIWALANI'' kwa Dar Es Salaam na Mikoani

Tuma pesa kupitia namba hizi kisha tuma sms yenye jina lako na mahali ulipo kwa msaada zaidi piga namba hii--0717254451

0 Comments:

SLOGAN YA ''TEAM RED SHISHA''

KWA MWENYE KUHITAJI T-SHIRT YENYE LOGO AU SLOGAN HII YA ''TEAM RED SHISHA'' TUWASILIANE KUPITIA MAELEKEZO HAYA RAHISI
LIKE PAGE YETU HAPA>>>https://www.facebook.com/pages/KIWA-WEE-ONe/1459825154247881?ref=hl

0 Comments:

''TRUE MEMORY'' Maarifa NAC feat Mbalamwezi Coming Soon

Hii ndo Cover Rasmi Ya wimbo mpya toka kwa MAARIFA NAC akimshirikisha  MBALAMWEZI Imefanyika Pale BIG SOUND Chini Ya Producer BANNY MUSIC............ COMING SOON

0 Comments:

KIWA WEE ONe Fashion

Ni wauzaji wa  T-shirt Zenye Slogan Ya Kiwa Wee One Baada Ya Team Kiwa Wee One Sasa Wamekuja na Slogan Nyingine Inaitwa ''TEAM RED SHISHA'' ni Kwa Mtonyo Wa Buku 15000/= tu wasiliana nao kwa namba 0716-721584 au 0719-115037/0654-841050 wapo kiwalani minazi mirefu

Muonekano wake huu hapa
kwa maelezo zaidi like page yao hapa>>>KIWA WEE ONe

0 Comments:

ULEVI WA STANZA

Pakua Wimbo Wa Last Mbihi Akimshirikisha Sirkiller MC na Man Kide
DOWNLOAD HERE>>>https://mkito.com/song/ulevi-wa-stanza-with-last-mbishi-na-man-kide/12872

0 Comments:

''MWENGE+KIWALANI'' [Old Shool Vibe] TAREHE 15 INATOKA

 Albam Ya P The MC na ZaiiD imepangwa kuachiwa mtaani tarehe 15 kama wasemavyo wenyewe kaa mkao wa kusikiliza na ku-support harakati ukiwa kama  shabiki mpenda harakati na mwenye kuijali harakati ni kwa mtonyo wa buku 5000/= tu za kitanzania

0 Comments:

KIWAMUZIK COMPANY

Hii ni kapuni inayojiusiha na utengenezaji wa Music hii ni moja kati ya music cover
  hii ni music cover                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                      
na hii ni moja kati ya banner ya blog kwa mwenye kuhitaji tupigie simu 0719-115037 tupo kiwalani minazi mirefu                                                                                                                                               

0 Comments:

Angalia video ya P THE MC


Angalia video ya P THE MC akiwa kilingeni akionyesha Uwezo wake

ANGALIA HAPA>>>

0 Comments:

SHARO MILIONEA HUJABUGI MEEN

MCHEKESHAJI aliyejitosa katika muziki wa Bongo Fleva na kujizolea maelfu ya mashabiki, Sharo Milionea ameaga dunia ghafla katika ajali mbaya ya gari iliyotokea Novemba 26, mwaka huu maeneo ya Songa-Maguzoni, Muheza mkoani Tanga.
Marehemu alikuwa akitokea Dar es Salaam kwenda Kijiji cha Lusanga, Muheza, Tanga ambako ni nyumbani kwao.

‘HUJABUGI MEEN’
Kifo kimeumbwa kwa kila binadamu na kila mmoja ana njia yake ya kuondokea. Sharo Milionea ameondoka kwa njia ya kupata ajali ya gari barabarani, kama mwenyewe alivyokuwa akipenda kusema ‘umebugi meen’, kufa kwake kwa ajali ‘hajabugi’ bali ni Mungu ameruhusu.
Mungu ana uwezo wa kuruhusu binadamu kuondoka duniani kwa njia yoyote ile, hata ya kukaa kwenye kiti na kufa.
Wote wanaokutwa na umauti kwa njia yoyote, hakuna aliyekosea bali Mungu anakuwa ameruhusu itokee hivyo.
KUMBUKUMBU YA KUSIKITISHA
Novemba 12, mwaka huu, marehemu alitoka kwenye gazeti ndugu moja na hili (Ijumaa Wikienda) katika safu ya Wikienda Star Shopping’ ambapo mastaa wa Bongo hupigwa picha wakifanya manunuzi katika maduka mbalimbali ya nguo, viatu nakadhalika.
Akizungumza na paparazi wa safu hiyo alipomnasa katika Duka la Robby One lililopo Kinondoni, Dar, Sharo alisema ili mtu awe sharobaro wa ukweli lazima asiwe mbahili katika kununua nguo kila wakati.
“Kweli kabisa ndugu yangu hutakiwi kuwa mbahili kwani ukiwa na tabia hiyo wavimba macho mitaani watakutungia jina la sharobaro mchafu,” alisema Sharo Milionea.
Komediani huyo alifanya shopping iliyogharimu kiasi cha shilingi za Kitanzania laki mbili na ushee.
HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Jina kamili ni Hussein Ramadhan Mkieti lakini alikuwa maarufu kwa jina la Sharo Milionea. Alizaliwa Machi 20, 1985 katika Kijiji cha Lusanga, wilayani Muheza Mkoa wa Tanga akiwa na pacha wake aitwaye Hassan.
Marehemu alipata elimu yake ya awali katika Shule ya Msingi ya Lusanga wilayani Muheza na kuhitimu mwaka 99.
ALIJITAMBUAJE KUWA NI MSANII?
Wakati akiendelea kukua kijijini kwao, Sharo alijitambua kuwa ni msanii kutokana na kutumia muda mwingi kufanya matukio yenye kuashiria ni mtu wa fani hiyo.
Mjomba wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, alisema Sharo katika utoto wake alikuwa akisumbua kwa kupenda kuandika kwenye kuta za nyumba.
NENO LAKE KICHWANI
Alisema miongoni mwa maneno aliyokuwa akipenda kuyaandika Ziro 5 lilikuwa likiongoza hali iliyokuwa ikimfanya anusurike kula kichapo kila mara kutoka kwa wazazi wake.
KUCHEZA NDIYO ZAKE
Mjomba mtu huyo aliendelea kusema kuwa wakati wa utoto wa kuanzia miaka 10 na kuendelea, marehemu alipenda kucheza bila aibu hata kama hakuna muziki uliokuwa ukipigwa.
MAZISHI YASHANGAZA WENGI
Marehemu Sharo Milionea alizikwa jana kijijini kwao, Lusanga, Muheza na kuhudhuriwa na maelfu ya watu. Katika kijiji hicho, mazishi ya Sharo ndiyo ya kwanza kuhudhuriwa na watu wengi tena kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina

0 Comments:

PAKUA MIZIKI YA ''Mika Mbwai'' Hapa.....

0 Comments:

Sasa pakua Albam Ya P The MC na ZaiiD inaitwa OLD SCHOOL VIBE [Mwenge+Kiwalani} kupitia mkito.com..Support yako ni Muhimu Sana


Download here>>>>https://mkito.com/artist-profile/p-the-mc-na-zaiid/1076                                                 

0 Comments:

PAKUA MIZIKI YA P The MC hapa

0 Comments:

Tazama Video mpya toka kwa LAST MBISHI .feat. MR:PERFUME-Nitrudi Mboka..chini ya Director CHIDY COMBO




0 Comments:

Pakua wimbo wa Sirkiller MC akishirikiana na wanandugu wawili ''MIKA MBWAI na MON G'' Wimbo unaitwa ''SAUTI YA HAKI''

0 Comments: